WAJUE WANYAMA WAKUBWA WATANO TANZANIA
1. TEMBO: Tembo ndiye mamalia mkubwa kuliko wote duniani, ana ngozi isiyo na vinyweleo, meno marefu na yaliotokeza kwe nje. Kuna spishi mbili za tembo moja ni tembo wapatikanao katika misitu na pia tembo wapatikanao katika vichaka. Tembo huishi katika familia ya makundi isiyo pungua tembo mia moja huku kiongozi wa familia akiwa ni tembo jike. 2. FARU: Faru ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi. Utofauti ya faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wananyodhani. Kwa bahati mbaya hivi sasa wanyama hao wamekuwa wakipungua kutokana na ongezeko la ujangili uliokithiri barani Afrika. Pembe ya faru inasadikika kutumika kama tiba ya magongwa mbalimbali hasa bara la Asia.Mwaka 2012 pembe ya faru ilikuwa ikiuzwa dola 60,000 kwa kilo. Tukiweza kuzuia ujangili ...